Our Blog
13
Mar
Njia Bora Za Kuongeza Mauzo

Njia Bora Za Kuongeza Mauzo

Author Digital wavesOn 13. Mar 2017

Mauzo ni uti wa mgongo wa kila shirika au kampuni. Hiki ni kitengo ambacho mapato yote hupatikana. Katika ulimwengu wa leo wa ushindani kila mmoja anakazana kutengeneza faida zaidi na kuwaridhisha wateja wake. Maelfu ya wauzaji wanakimbizana barabarani kushawishi wateja wao kununua bidhaa zao au huduma wanazotoa.

Litambue Soko Lako

Ni muhimu kutambua watu gani hasa ni walengwa wa bidhaa yako. Kama unauza vitabu basi walengwa hasa ni Mashule na makampuni. Kama huduma yako ni kutafuta masoko kwa mtandao basi ni muhimu kutambua ni watu gani wanaweza kukulipa kulingana na huduma unayotoa.

Andaa Mpango Halisi Wa Mauzo Yako

Hii ni pamoja na malengo yako kwa mwezi au robo mwaka. Unampango wa kupiga simu ngapi kwa watu usio wajua kabisa au unampango wa kutembelea watu wangapi kwaajili ya mauzo. Andaa sehemu unazotegemea kutembelea mapema ili kupunguza gharama za usafiri. Weka malengo ya mwezi.

Kuwa Na Bidhaa Chache Kama Sampo

Wateja huchagua sana. Wanaweza kuuliza maswali elfu kabla ya kununua kitu. Hivyo ni busara kuwa na sampuli ya bidhaa zako au hata kutoa muda wa majaribio kwa mteja kutumia na kuona faida zake. Ukiweza kumfurahisha mteja ni sawa na mauzo yamefanyika kwa asilimia 80.

Fanya Majadiliano Kwa Akili Na Funga Mikataba

Wateja mara nyingi husema “hatuna hio pesa tunauwezo wa kulipa pesa kadhaa tu” hapa inabidi uwe makini na bei yako na kukubali pungufu pale unapoona inawezekana tu. Saa zingine unaweza kuanza na bei ya juu kidogo ili wakitaka pungufu uweze kufikia ile bei stahiki ya bidhaa au huduma hio.

Kwa kutumia mbinu hizo zilizotajwa hapo juu. Watu wa mauzo wanaweza kufikia malengo yao na kuongeza mauzo kiujumla. Lakini pia ni muhimu kujiwekea nidhamu katika kazi ili kuhakikisha mauzo yanafanyika. Tofauti na muundo wa bidhaa yako ni jinsi unavyoitambulisha kwa watu na faida zako.

Created with Snap