Our Blog
6
Feb
Jinsi Ya Kuongoza Watu Wa Mauzo

Jinsi Ya Kuongoza Watu Wa Mauzo

Author Digital wavesOn 06. Feb 2017

Kama meneja kazi kubwa ambayo wengi hupata ni kuhakikisha watu wamauzo wanafanya kazi nzuri. Mara nyingi tunawalaumu wafanyazi wenzetu kwa matokeo yasiyo ridhisha kama kutokuwa na mpangilio, mipango, kughairi mambo, kutokuwa na ushirikiano, mauzo sifuri na mengine mengi.

Hata hivyo kama maneja inabidi tuwe makini katika mbinu zetu tunazotumia kuongoza timu zetu. Nahodha anaweza kuzamisha meli au kuiongoza mpaka ufukweni.

Ni muhimu kuweka akilini kuwa timu yako ndio mafanikio au hasara yako. Jinsi unavyopanga kuunda na kuongoza timu yako ndio kutaleta matokeo katika ushalishaji.

Njia za kuongoza watu wa mauzo ni kama;

  • Tumia njia ya ufundishaji, kuwaongoza na kuwaelezea bila kuwa na matarajio makubwa katika uwezo wao. Kama maneja unatakiwa kutambua kuwa sio kila mtu anaujuzi au uzoefu mzuri kufanya mauzo. Ongea nao namna ya kutatua matatizo wanayokutana nayo bila kukasirika. Mnaweza pia mkajadili changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika kufanya mauzo. Kuwa nao pamoja katika kila hatua.

 

  • Fanya urafiki na wafanyakazi. Watu wa mauzo sio kama wahasibu au wanyakazi wengine katika kitengo chako ambao wanafuata utaratibu Fulani kufanya kazi. Watu wamauzo wananamna zao pekee zakuwashawishi wateja kununua bidhaa hizo. Huwezi kumlazimisha mtu wa mauzo kutumia njia unayomuelekeza kushawishi wateja kununua. Timu yako inahitaji kuwa huru kutumia uwezo wao kufanya mauzo.

 

  • Tambua uwezo wa kila mtu katika timu yako. Kwa mfano; mwengine anaweza akawa sio mzuri katika kuandaa mikakati au ripoti. Lakini anaweza kuwa mzuri katika kumshawishi mtu na jinsi yakuwasilisha bidhaa kwa mteja.

 

 

  • Kuwapongeza; Moja ya njia mbadala yakufanya timu yako iendelee kufanya kazi vizuri ni kuwapongeza. Ikiwa ni mauzo kwa mara ya kwanza au ya mia. Ni lazima kuonesha umuhimu wa kazi anayofanya mtu wa mauzo. Kuna wakati ambapo mauzo yako chini sana. Hii inaweza kusababishwa na hali mbaya ya uchumi, mabadiliko ya hewa, siasa na mengineyo. Kama meneja bado unatakiwa kuonesha unatambua jitihada zao za kuongeza mauzo ya kampuni.

Created with Snap